NYAKAHANGA DD HOSPITAL YATUNUKIWA CHETI CHA UTAMBUZI NA NHIF NA KUSHIKA NAFASI YA PILI MKOANI KAGERA. Comments: 1

image

Author names: Denice Shumbusho saved date: 2026-25-10 at 15:10

Tarehe 21 Oktoba 2026, katika hafla ya uzinduzi wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashai, Bukoba, Nyakahanga DD Hospital ilitambuliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa mchango wake katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii kupitia bima ya NHIF. Katika hafla hiyo, hospitali yetu ilikuwa miongoni mwa taasisi zilizotunukiwa vyeti maalum vya utambuzi kwa mchango wao katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi. Katika hafla hiyo, hospitali yetu ilifanikiwa kushika nafasi ya pili kwa Mkoa wa Kagera, ikitanguliwa na Hospitali ya Mkoa (BRRH). Mafanikio haya yanaonesha juhudi, kujituma na dhamira yetu ya kuendelea kuboresha huduma za afya kwa jamii. Cheti hicho kilikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Kanali Yahaya Ramadhani Kido, na kupokelewa na Dr. Furaha Kahindo, Mganga Mkuu wa Nyakahanga DD Hospital. Utambuzi huu ni chachu ya kuendelea kuboresha huduma zetu na kutekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma za afya zenye weledi na ubora kwa kila mwananchi. 🙏 Tunatoa shukrani kwa NHIF kwa kutambua mchango wetu. Tunaendelea kujituma kwa ajili ya afya bora ya jamii yetu.

Lasts news/event

SHEREHE ZA MEI MOSI

Bw Sylidion P. Karugaba akipokea cheti cha Mfanyakazi Hodari katika viwanja vya Posta Ngar...

MFANYAKAZI HODARI 2025

Kwa mara nyingine tena Hospitali ya Nyakahanga imepata mfanyakazi hodari Bw Sylidion P. Ka...

See all news / events

Contact info

DOCTOR IN CHARGE
NYAKAHANGA DESIGNATED DISTRICT HOSPITAL
PO BOX 110, KARAGWE VIA BUKOBA, KAGERA

Phone +255 767 084 362/ +255 787 663 565 (Medical officier Incharge)
+255 756 069 466/ +255 622 736 736 (Hospital Secretary)